Chorus
Kumekucha - ni siku kubwa ya ajabu leo hii
Kumekucha - ni siku ya furaha na amanin{ Watu wote - wanameremeta, tazama
Wamevaa - mavazi mazuri oneni
Nyuso zao - tabasamu shangwe nderemo na vifijo } *2
Verse 2
[ s ] Pokeeni bahati yenye upekee
Kufurahiya pendo lisilo dosari
La mwenyezi Mungu mwema na mkari-mu
Verse 3
Heri gani ndugu tumejaliwa leo
Kusimama pamoja tukiwa na hamu
Kuyashuhudia makuu ya le-o
Verse 4
Tupaze sauti wote watusikie
Watakaoweza wajumuike nasi
Shangwe nderemo chereko na vifi-jo