SectionsExitKulea Watoto

Kulea Watoto

Ordinary Time,Ordinary TimeExit
Chorus

Kulea watoto ni kazi ya baba na kazi ya mama

Hilo ndilo jukumu walilopewa na Mwenyezi Mungu

Na kazi hiyo ifanywe kwa msaada wake Muumban

Ni kwa nini tunawanyima malezi bora na ya muhimu?

Ni kwa nini tunawabembeleza watoto manyumbani?nn{Watoto wanahitaji malezi yaliyo mema

Ni lazima waonyeshwe njia bora ya kupita

Ili kuwafurahisha wazazi na baadaye taifa}*2

Verse 2

Angalia watoto wadogo wanavyozurura

Usiku kucha utafikiri kwao ni mchana

Waone watoto wanavyofaa wengine nusu uchi

Mbele ya jamii pia na kwa wazazi wao

Verse 3

Mtoto anahitaji kupata angali mbichi

Ili aweze kukua katika maadili mema

Wazazi acheni pia kuwalea watoto kitajiri

Na kuwapa pesa nyingi eti ni za matumizi

Verse 4

Pesa za watoto zinaishia kununua bangi

Kununulia kila aina ya dawa za kulevya

Tunadhani tunawapenda watoto kumbe tunawaharibu

Tujirekebishe wazazi tuokoe watoto