Kuimba Ni Raha
Ordinary Time,Easter,Lent,Ordinary TimeThanksgiving
Chorus
Ni raha ni raha kuimba ni raha
Kumwimbia Bwana
Ni raha ni raha kuimba ni raha
Kumwimbia Bwana
Verse 2
Pazeni sauti wapendwa imbeni
Mtatambua ilivyo raha
Tangazeni sifa za Bwana popote,
Ni baraka na ni raha sana jamani
Verse 3
Sauti zetu zikifika kwa Mungu,
Malaika wataimba raha
Nazo zikimpendeza atashusha,
Heri neema na raha sana jamaani
Verse 4
Tukimwimbia kwenye shida na tabu
Anatuhurumia sana
Kwenye huzuni ataleta faraja
Nguvu amani na raha sana jamani
Verse 5
Kwenye mafanikio tunayopata
Tumshukuru kwa nyimbo Bwana
Atazidisha baraka zake kwetu
Tudumu katika raha sana jamani