Verse 1
Kristu Paska yetu, amechinjwa sadaka;ntuile karamuye, na twimbe Aleluya
Verse 2
Aliyejitoa, sadaka ya Paska,nwakristu wamtolee, sadaka ya Sifa.
Verse 3
Mwanakondoo aliwakomboa kondoo, Kristu asiye na dhambinamewapatanisha na Baba, watu wenye dhambi.
Verse 4
Mauti na uzima, vimeshindana ajabu;
Mkuu wa uzima aliyekufa, atawala mzima.
Verse 5
Utuambie Maria, uliona nini njiani?
Niliona kaburi la Kristu Mzima,nna Utukufu wa aliyefufuka.
Verse 6
Mashahidi ni Malaika,
Leso ya uso na mavazi
Kristu tumaini langu kafufuka,nawatangulia Galilaya.
Verse 7
Twajua Kristu amefufuka, kweli katika wafu
Ewe Mfalme mshindaji, Utuhurumie.
Verse 8
Amina Aleluya, Amina Aleluya *2