Kivumbi

Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Lent,Christmas,Ordinary Time,Resurrection,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Easter,Christmas,Ordinary Time,Ordinary Time,Christmas,Ordinary TimeThanksgiving
Verse 1

Hapo ndipo tulipomfurahia Bwana Mungu wetu

Hirizi na mizimu yote viliposhindwa kusimama

Shetani naye kivumbi kakitimua kakimbia

Chorus

{Hapo ndipo tukasema hebu Mungu aitwe Mungu

Hapo ndipo tukasema yeye apewe sifa

Hapo ndipo tukasema atawale Mungu milele } *2

Verse 3

Tazama Bwana alipounyoosha mkono wake mkuu

Wachawi wote wakakoma, mapepo na yakanyamaza

Waganga na tunguri zao kwa aibu wakaduwaa

Verse 4

Bwana alipoinua mkono hodari kwa wagonjwa

Wakoma wakatakasika viziwi wakasikia

Viwete wakarukaruka kwa furaha wamepona

Verse 5

Jicho la Bwana lilipowaelekea watu waovu

Hasira, chuki na majivuno vyote vikatoweka

Kiburi na maringo yao hapo ndipo vikapotea