Kimya kimya ni cha nini Bwana Yesu ametualika
Kushiriki karamu yake, karamu ya mapendo
Siku ile iliyotangulia kifo chaken(Aliwaita wanafunzi wake) *2 akawaambia
Huu ndio mwili wangu utakaotolewa kwa ajili yenu
Kuleni huu ili mpate uzima wa milele,n(Haya basi amkeni (‘mke-ni) ‘mkeni basi amkeninkushiriki uzima mtukufu kwa karamu ya Bwana }*2
Hii ndiyo damu yangu itakayotolewa kwa ajili yenu
Kunyweni hii ili mpate uzima wa milelen(Haya basi amkeni (‘mke-ni) ‘mkeni basi amkeninkushiriki uzima mtukufu kwa karamu ya Bwana }*2
Amini ninawaambieni alaye mwili na kunywa damu
Bila kustahili atahukumiwa siku ya mwisho,
Lakini alaye mwili na kunywa damu kwa kustahili
Nitamfufua siku ya mwishon(Haya basi amkeni (‘mke-ni) ‘mkeni basi amkeninkushiriki uzima mtukufu kwa karamu ya Bwana }*2