SectionsEntranceKimya Bara Na Bahari

Kimya Bara Na Bahari

Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Lent,Christmas,Ordinary Time,Resurrection,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Easter,ChristmasEntrance
Verse 1

Kimya bara na bahari, kimya mbingu na dunia

Bwana na Muumba wenu, mtoto Yesu asinzia

Chorus

Kimya, kimya, asinzia, mpenzi wetu mtoto Yesu * 2

Verse 3

Amelazwa manyasini, mchanga mkiwa, myonge pia

Yosefu na Maria wamo, mtoto Yesu kumtunzia

Verse 4

Malaika wanashuka, mfalme wao kumlindia

Wanatunga nyimbo nzuri, mtoto Yesu kumwimbia

Verse 5

Wachungaji waja mbio, kwa mshangao waingia

Waanguka magotini, mtoto Yesu kumuabudia

Verse 6

Nasi pia twende hima, Mungu wetu kumwangalia

Twende sote kwa juhudi, mtoto Yesu kumwamkia