SectionsEntranceKimeeleweka

Kimeeleweka

Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Lent,Christmas,Ordinary Time,Resurrection,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,EasterEntrance
Chorus

Kilichomfanya Baba amtoe mwanawe wa pekee

Kilichomfanya mwana akubali kufa kifo cha aibu

Leo kimefafanuliwa, leo kimeeleweka

Leo kimefafanuliwa, kimeeleweka, kimeeleweka!

Verse 2

Alimuona mwanadamu, anaanguka kuzimu

Akaja kumuinua, akakibugia kifo

Akashuka nacho, kuzimu kisha, akakiacha huko

Verse 3

Alijua udanganyifu wa Ibilisi mzushi

Akaja kuuharibu na kufunua ukweli

Kuzigaragaza, hila za mwovu, na kumuaibisha

Verse 4

Alimpenda mwanadamu, akampenda upeo

Kajifanananisha naye bali hakutenda dhambi

Akamuinua kiumbe huyu kampandisha hadhi

Verse 5

// h i t i m i s h o //

Amevishinda vita vya imani, mshindi

Amevaa utukufu na enzi, Mwokozi

Aeh atangaza mlango wa mbingu, u wazi

Aeh na urithi wa utawala

Verse 6

Kafufuka kama alivyosema yesu,

Amefufuka, ameyashinda mauti

Kafufuka (kafufuka) kama alivyosema Yesu,

Amefufuka (kafufuka) ameyashinda mauti

Verse 7

Kaivunja milango yote ya kuzimu,

Ameivunja, ameyashinda mauti, kafufuka . . .

Verse 8

Kaonyesha ya kwamba inawezekana,

Ameonyesha ameyashinda mauti, kafufuka . . .

Verse 9

Kwa hiyo, tuimbe aleluya ni shangwe kuu,

Kwa hiyo, tuimbe aleluya kwani Bwana ameyashinda mauti

Kwa hiyo, tuimbe aleluya ni shangwe kuu,

Kwa hiyo, tuimbe aleluya kwani Bwana ameyashinda mauti

Verse 10

Ameyashinda mauti, ameyashinda mauti,name ame ame ame ameyashinda mauti