SectionsExitKilio Cha Mjane

Kilio Cha Mjane

Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Lent,Christmas,Ordinary Time,Resurrection,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary TimeExit
Chorus

Ni nani wa kuwasaidia na kuwajali wajane

Ni sisi tuliowapenda walipokuwa na waume zao

Ni nani wa kuwasaidia na kuwajali wajane

Ni sisi tuliowapenda na sasa tunawadhulumu hao

Verse 2

{Tazama leo ni sisi wenyewe chanzo cha huzuni kwao

Tazama leo ni sisi wenyewe chanzo cha machozi yao } *2n{ Ni nani atakayekisikiliza kilio cha mjane

Ni nani atakayekijali kilio cha mjane } *2

Mlishirikiana nao vizuri walipoifunga ndoa yao

Tazama bibi harusi walimkaribisha kwa nderemo

Nderemo nderemo tushangilie kaka yetu leo kapata jiko

Karibu karibu wifi karibu karibu hapa ni kwako

Verse 3

Maisha mazuri maisha magumu ilikuwa ni siri ya wawili

Maisha kufanikiwa hiyo ni siri ya baba na mama

Maisha ya ndoa yakitenguka baba mwenye nyumba akitutoka

Hatamu tunaishika kuchukua mali za marehemu

Wewe utachukua gari lile, mashamba yake mimi nitayatunza

Na nyumba ya marehemu ataisimamia kaka yetu

Mama na watoto tunafukuzwa thamani ya utu wetu haipo

Verse 4

Wengine wanachukua watoto wa marehemu wakawasomeshe

Na kumbe ni hila tupu wanafanyizwa kazi ngumu ngumu

Kupika na kudeki kazi yao kufua nguo hata na kupasi

Huruma itakujia ukiwaona wanavyotetesha

Ndugu yangu leo ninakuomba mimi nawe sasa tubadilike

Na tuwe kitu kimoja mfano wa kuigwa na jamii

Tuonyeshe na kudhamini haki za wajane hata na kuwajali

Watoto tuwajengee misingi bora ya baadaye