SectionsEntranceKilio Cha Damu

Kilio Cha Damu

Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Lent,Ordinary Time,Ordinary Time,Advent,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,LentEntrance
Chorus

Mate yakamkauka, moyo ukaganda,

Na akakumbuka hali ya bustani Getsemani

Mwili wake ulipotona jasho la damu

Ngozi ikasinya, roho ikalia

Na akang'ata meno kwa maumivu makali

Kovu za misumari zilipouma upya

Maisha ya vijana wa leo, yanatonesha majeraha ya Yesu

Yale matendo yamo kwa giza, yanamliza kilio cha damu

Verse 2

Akatazama kwenye kwenye vijiwe

Vijana wamevuta wamelewa

Kaona nyumba za wageni

Wenyeji wanagawana ukimwi

Verse 3

Kwa zahanati kuna foleni

Vijana wanavinyonga vichanga

Usiku kucha, dodo mapanga

Vijana watafuta utajiri

Verse 4

Wengine hao barabarani

Wanauza hekalu la Roho Mungu

Kisigizio, ajira haba

Wateja wao ni wazazi wao

Verse 5

Na majasira wanageuza

Miili yao kufanya mabomu

Wakidanganywa ati dhawabu

Kumbe adhabu wanajitwalia

Verse 6

Tubuni sana salini ninyi

Jahazi lenu limeshatoboka

Ombeni yeye awahifadhi

Kwenye tundu la ubavuni mwake