SectionsExitKila Kunapokucha

Kila Kunapokucha

Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Lent,Christmas,Ordinary Time,Resurrection,Ordinary Time,Ordinary TimeExit
Chorus

{ Kila kunapokucha, ndugu zangu mimi

Wananikwepa na kunikimbia

Majirani zangu wanatazamana bila kunitamkia neno

Ewe Muumba wangu najiuliza na kujitafakari mimi

Au nimekuwa na sura ya simba,

Au nimekuwa na sura ya chui, hata ninatisha } *2

Verse 2

Ninapokaa chini na kutafakari mwenendo wangu

Kwani uko vipi mimi niliupenda,

Japo magumu mimi niliyapata,

Nilivaa sura ya kifalme pasipo kuwa na utu

Verse 3

Nikiupekua pekua moyo wangu unanitisha

Ni huo tena kwa kudhamiria

Kwa kauli toka kwa ulimi wangu

Nilifanana na jitu baya tena limezalo watu

Verse 4

Hakuna adui hakuna rafiki kwangu wote sawa

Hakuna mwema katika moyo wangu

Wala rafiki katika roho yangu

Nilijifananisha na chui tena chui mwenye njaa