Chorus
{ Kikondoo cha Mungu, mkate wa Mbinguni
Mlishi wa roho zetu, nakuabudu }*2
Verse 2
U Babangu mwema, na msimamizi
Mpaji wa uzima, wangu mwokozi
Verse 3
Fumbo abudiwa, nakuamini
Kaza Yesu mpendwa, yangu imani
Verse 4
Mlo wa roho yangu, hostia nzima
Niwie ya mbingu, kweli amana
Verse 5
Ee Rabbi mtu Mungu, unirizishe
Njoo shuka kwangu, kanishibishe
Verse 6
Anakaribia, mpenzi amini
Ataka ingia mwangu moyoni