Kidole Juu

Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Lent,Ordinary Time,Ordinary Time,Advent,Ordinary TimeThanksgiving
Verse 1

Hayo mliyofunuliwa, bila kuyalipia kitu,

Nayo ndiyo yale mliyotumwa,

Kwenda kwa walio wadogo

Mungu alowatunukia awe mkuu peke yaken(Jiulize) nani kwenu (aliyeomba) kuzaliwa!n(Jiulize tena) nani kwenu (anayejua) siku ya kufa!

Hakuna! Hakuna! ha!

Chorus

Hakuna jambo mnalomiliki hapa duniani

Yote mliyo nayo yana mwenyewe mnamjua

Naye amewapa haya kusudi mtumikiane

Ili kusiwepo na matabaka miongoni mwenu

Hiyo ndiyo hekima - eeh aah eeh

Hiyo ndiyo hekima - eeh aah eeh

Ndugu hiyo ndiyo hekima ya kweli } *2

Verse 3

Kama mliyo nayo yote yangekuwa yenu

Hiyo pumzi mnayojivunia wapendwa,

Isingekuwa inakiogopa kichomi

Ingeendele-a hata palipo kichomi!

Verse 4

Uzuri wa sura zenu zenye ngozi laini

Inakuwaje hamuwezi kuuelekeza,

Usiungue hata kwenye maji ya moto

Na usioze unapolala kaburini!

Verse 5

Elimu na vyeo vyenu na mamlaka yenu

Akili nyingi ufundi navyo vipaji vyenu,

Mbona hamvitumii nyi mkiwa usingizini

Na mnaota ndoto sawa na za watoto!

Verse 6

Basi mimi, ninahimizwa, kujiepusha, kujiinua

Nijishushe, mbele ya wote,

Wawe wakubwa, au wadogo

Nisijiinue kati ya watu hata siku moja,

Badala yake nijinyenyekeze ili nifikike,n

Akihitajika atakayewatumikia watu

Niinue kidole juu kusudi wanitume mimi, daima

Kidole juu kusudi wanitume mimi

Kidole juu, kuitikia wito daima

Kidole juu, kusudi wanitume mimi

Na nikitumwa niwe mwaminifu daima

Kidole juu, kusudi wanitume mimi

Kidole juu wanitume na Mungu atukuzwe daima

Kidole juu, kusudi wanitume mimin

Kidole juu, kidole juu, leo

Kidole juu, kusudi wanitume mimi

Kidole juu, kidole juu, daima

Kidole juu, kusudi wanitumie mimi, milele!