SectionsExitKama Vile Mwili

Kama Vile Mwili

Ordinary Time,Ordinary TimeExit
Chorus

{Kama vile mwili ni mmoja nao unao viungo vingi

Tena na viungo vyote vya mwili ulonavyo ni vingin(Kweli) Ni mwili mmoja }*2n{Vinafanya kazi zote, kwa pamoja siku zote

Kwani vyote vya maana, na vizuri kwelikweli

Nasi sote Wakristu tushirikiane }*2

Verse 2

Kwa maana katika Roho, sisi sote tulibatizwa

Tulinyweshwa Roho mmoja, basi sote ni mwili mmoja

Verse 3

Kama sisi ni Wayahudi au sisi ni Wayunani

Tukiwa ndani ya Yesu hatuko tofauti kabisa

Verse 4

Miguu, mikono na macho masikio hata mapua

Na viungo vyote vya mwili vinafanya kazi kwa pamoja

Verse 5

Katika kanisa la Bwana sisi sote tuna nafasi

Tutumie nafasi zetu kwa huduma ya kanisa lake