SectionsExitKama Kunguru

Kama Kunguru

Lent,Ordinary Time,Marian,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Easter,Lent,Easter,Christmas,Ordinary TimeExit
Chorus

{ Kama kunguru arukapo juu ya jalala kubwa

Akitafuta mizoga na wadudu

Alishibishe tumbo lake } *2nn{ Ndivyo moyo wake mtu asiyempenda Mungu

Utakuwa wa kubabaika na kuhangaika

Hatakuwa na amani,

Atakuwa kama kunguru tu, kama kunguru tu,

Awindaye toka macheo ya jua hata yapata mawio

Na tumbo lake bado ni tupu } *2

Verse 2

Moyo wako ndugu mbona waubabaisha,

Kutwa kucha wewe umemsahau Mungu

Dunia ina mambo yake - tena yanapita

Verse 3

Kama una kiu na tamaa za dunia

Zina mwisho wake kwanza mtafute Mungu

Mungu alishapanga yako - hivyo umuombe