SectionsExitKaeni Katika Pendo

Kaeni Katika Pendo

Wedding,Wedding,Ordinary TimeExit
Chorus

Kama vile Baba alivyonipenda mimi

Nami nilivyo wapenda ninyi

Kaeni katika pendo langu

Kaeni - katika pendo (langu) * 2

Kaeni katika pendo langu

Verse 2

Mkizishika amri zangu, mtakaa katika pendo langu

Kama vile mimi nilivyozishika, amri za Baba yangu

Na kukaa katika pendo lake

Verse 3

Hayo nimewaambia, ili furaha yangu iwe ndani yenu

Na furaha yenu itimizwe

Verse 4

Amri yangu ndiyo hii, mpendane kama nilivyowapenda

Kama nilivyowapenda ninyi

Verse 5

Hamna aliye na upendo, upendo mwingi kuliko huu

Wa mtu kutoa uhai wake, kwa ajili ya rafiki zake