Chorus
{ Kabila langu nimekutenda nini
Au nimekusikitisha nini, nijibu, nijibu } *2
Verse 2
Kwa kuwa nimekutoa katika nchi ya Misri
Umemtayarishia mkombozi wako msalaba
Verse 3
Kwa kuwa nimekuongoza jangwani kwa miaka arobaini
Umemtayarishia mkombozi wako msalaba
Verse 4
Ilinipasa kukutendea nini zaidi nisikutendee
Kweli nimekupenda kama shamba langu nzuri sana
Verse 5
Mimi nimewapiga Wamisri kwa ajili yako,
Nawe ukanitoa nipigwe mijeredi.
Verse 6
Mimi nimekutoa Misri, nikamtoa Farao katika bahari ya Sham,
Nawe ukanitoa kwa makuhani wakuu.