Johera

Marian,Lent,Advent,Ordinary TimeEntrance
Chorus

Johera ( dakunyi's herahera)*2

Manyase endwaro wololo hawawene

Johida (dakunyi's hidahida )*2

Manyase endwarowololo niwakadhi

Njooni wote tushangilie,n{Tuimbe kwa furaha, tucheze bila mwisho,

Tutoe shukrani kwa Bwana mtawala }*2

Verse 2

Waumini simameni, mbele zake Mungu wetu

Waimbaji mziimbe, sifa zake Jehova Rama

Waumini tamkeni, utukufu wake Yahweh

Makasisi na watawa na wacheze nyumbani mwakenshangwe

Verse 3

Kwa sauti ya kinanda, kwa filimbi na kayamba

Kwa kinubi na kwa zeze, tunamwimbia Mungu wetu

Kwa kelele za furaha, kwa makofi kwa machezo

Kwa vigelegele kweli, njooni nyote tutoe shukrani

Verse 4

Mwimbieni Mungu wetu, mwimbieni wimbo mpya

Mwimbieni kwa furaha mwimbieni kwa shangwe kubwa

Mungu wetu ni mkuu, ametenda maajabu

Ameumba vitu vyote, ulimwengu na jeshi lake lote

Verse 5

Mungu wetu katuumba, ili sote tumjue

Sisi sote tumpende, tumtumikie daima

Ametupa vitu vyote,atulinda siku zote

Tuna heri ya milele, tutaishi mbinguni kwake Baba