Chorus
Jipe moyo Bwana yuko nawe, (tena)
Hakuachi kamwe kwani yeye akupenda
Hata shida zikikuandama (ndugu)
Umtegemee, Yesu atakuongoza
Verse 2
Njia imejaa giza na umande,
Huku watembea bila hata nuru wasi wasi
Hofu yakujaa woga watawala
Wasimama wima hujui pa kwenda
Ushujaa watoka wabaki upweke,
Bali yu pamoja na wewe
Verse 3
Ndugu watoweka wakuacha pweke,
Hata marafiki uliothamini watoroka
Hofu yakujaa woga watawala
Wasimama wima hujui pa kwenda
Ushujaa watoka wabaki upweke,
Bali yu pamoja na wewe
Verse 4
Kila utendacho, hakiwezekani,
Wajaribu sana kufaulu wala hauwezi
Hofu yakujaa woga watawala
Wasimama wima hujui pa kwenda
Ushujaa watoka wabaki upweke,
Bali yu pamoja na wewe