SectionsExitJicho Langu

Jicho Langu

Ordinary Time,Ordinary TimeExit
Chorus

Ni wewe jicho langu nakutegemea kuniongoza (niendapo)

Ni wewe jicho langu taa yangu ya kumulika njia (nipitayo)n{Niongoze kwa huruma, niongoze kwa mapendo

Nitazame mambo mema, yanayopendeza Mungu

Jicho langu niongoze hata nikafike kwa Mungu Baba}

Verse 2

Ukiwaona vipofu wote – tazama kwa huruma

Na ukiwaona walemavu wote . . .

Na ukiwaona wasiojiweza . . .

Nikafike kwake Mungu kwa huruma yangu

Verse 3

Ukiwaona yatima wote – tazama kwa huruma

Na ukiwaona na wajane pia . . .

Na ukiwaona wanaoonewa . . .

Nikafike kwake Mungu kwa huruma yangu

Verse 4

Mwenendo mbaya wa binadamu – hayo usitazame

Kama tamaa anasa ushirikina . . .

Na matendo yanayomuasi Mungu . . .

Nikafike kwake Mungu kwa matendo mema

Verse 5

Pia unapowaona wahitaji – tazama kwa upendo

Na kila mwanadamu aliyeumbwa . . .

Haja za familia uliyonayo . . .

Nikafike kwake Mungu kwa upendo wangu