SectionsThanksgivingJeshi La Malaika

Jeshi La Malaika

Ordinary TimeThanksgiving
Verse 1

Sasa jeshi la malaika lashangilia jina hili tukufu

Na sisi viumbe duniani twashuhudia utukufu mkuu

Twaungana na malaika tukisifu sana jina hili ni kuu

Tangu Yohane atabiri na sisi sote hatuliasi ni kuu

Chorus

Twimbe twimbe tumsifuni Yesu, jina lake latenda makuu

Mfalme Kristu mwana wake Mungu

Tumsifuni tumsifuni tumshukuru Mungu

Verse 3

Dhambi yake Adamu babu na bibi Eva ilikuwa asili,

Mkombozi Yesu katumwa dunia yote sisi kutuokoa

Waliokuwa na kiburi ni ibilisi na wenye shingo ngumu

Wamebaki midomo wazi wakiteketea kwa moto mkali

Verse 4

Wasioamini na wasiomkubali kwao ni kama ndoto,

Muda wao ukishapita kilio chao mavuno ni mkaa

Mawazo yao duni sana na mbinu zao zisizoenda mbali,

Wasiokubali ya kuwa Mungu ndiye mweza wa kila kitu

Verse 5

Kina Baba mama vijana pia watoto jueni hili jambo

Dunia yote ina mwisho ya duniani ni ya muda mfupi

Biashara zisiwe nyingi mkasahau aliyetuumba sisi,

Mwenye uwezo wa kutoa pumzi na afya yapaswa tumtii