Chorus
Je Bwana nastahili kujongea meza yako?
Je Bwana nastahili kujongea meza yako?
Kwani mimi si mnyofu wa moyo nifanye nini
Bwana ninatamani Nifanye nininnami nijongee meza yako Bwana nipate uzima wa milele
Verse 2
Njooni kwangu nyote, msiogope
Njooni mimi ni uzima wa milele
Verse 3
Njoo mwenye njaa usiogope
Mwili wangu ni chakula cha uzima
Verse 4
Njoo mwenye kiu usiogope
Damu yangu ni kinywaji cha uzima
Verse 5
Njoo mwenye dhambi usiogope
Kwani mimi ni wokovu wa milele