Chorus
{ Itengenezeni njia ya Bwana, Bwana apite (mapito yake)
Yanyoosheni mapito ya Mungu wetu aingie } *2
Verse 2
Tazama namtuma mjumbe wangu, mbele ya uso wako,
Atakayeitengeneza njia yako,
Sauti ya mtu, aliaye nyikani nyikani inasema *2
Verse 3
Ondoka ee Yerusalemu, usimame juu
Tazama uione furaha,
Inayokujia, kutoka kwake Mungu, Mungu wako *2
Verse 4
Yajazeni yale mabonde yote yashusheni milima,
Panyosheni na pale palipopotoka
Tayarisheni njia na mapito ya Bwana aingie *2
Verse 5
Na watu wote wenye mwili, wataona wokovu,
Wataona wokovu wake Mungu wetu,
Kwa sababu yeye atakayetukujia ni mwokozi *2