SectionsExitIsemavyo Torati

Isemavyo Torati

Ordinary Time,Ordinary Time,Lent,Resurrection,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Lent,Lent,Ordinary TimeExit
Chorus

{ Isemavyo torati ya kale, jicho kwa jicho, jino kwa jino

Mkuki kwa mkuki, hiyo silaha ya mababu } *2n{ Lakini mimi, ninawaambia, nawaambia,

Msilipize kisasi kwa mambo haya } *2n

Akupigaye shavu lako moja, mgeuzie na la pili

Akunyang'anyaye na joho lako -

Mpe pia kanzu yako, utayashinda majaribu.

Verse 2

Ndugu nawaambia nyinyi, jifunzeni kusameheana

Acheni chuki ubinafsi, hazisaidii kwa vyovyote.

Ukikosewa samehe, sababu hata wewe wakosea

Mungu asingesamehe, wewe na mimi tungekuwa wapi

Verse 3

Wewe unayemchukia huyu, huyu ameumbwa naye Mungu

Kumbuka wote sisi twapita, hakuna aishiye milele

Wamuua huyu na wewe, utakufa siku moja kama yeye

Utajibu nini kwa Mungu, kuifanya kazi yake bila ruhusa

Verse 4

Riziki aitoa Mungu, acha wivu pia masengenyo

Mwenzako amepata kwa jasho, fanya bidii ufanikiwe

Wamwonea wivu kwa nini, na kuanza kuharibu na kuiba

Utajibu nini kwa Mungu, kuharibu nchi yake aliyoumba