Nimefungua vitabu vyote nikapekua kurasa zote
Kulitafuta andiko hili sikuliona
Ni wapi palipohalalishwa matendo hayanmachafu sana yachafuayo jamii yetu sikupaona
Fungua macho mkristu, fungua macho
Giza nene limetanda, fungua macho
Ni wakati wa kukesha, fungua macho
Shetani katuzunguka, fungua macho
Imeandikwa wapi kwamba ushoga ni halali?
Wapi palipoandikwa rushwa ni funguo ya haki?n(tena) Imeandikwa wapi kwamba hirizi ni halali?
Wapi imehalalishwa wanaume kufunga ndoa?n(hiyo) Imeandikwa wapi, imeandikwa wapi?
Kurasa zote hakuna!
Imeandikwa wapi imeandikwa wapi?
Sheria zake Mungu!
Kemea Mkristu matendo hayo
Kwa sakramenti zote uyasafishe
Epukana nayo matendo hayo
Kwa sakramenti zake uyasafishe
Ingia katika shamba la Bwana
Mambo ya ulimwengu ni machafuko
Tembea katika shamba la Bwana
Zitende kazi zake kwa moyo safi
Njia zake Bwana usiziache
Ni barabara safi zenye amani.
Sheria za Bwana usiziache
Na maagizo yake ni ya Adili