Imani Yangu

Ordinary Time,Ordinary Time,Lent,Lent,Lent,Ordinary Time,Marian,Christmas,Ordinary Time,Lent,Lent,Ordinary Time,Wedding,Ordinary Time,Ordinary Time,Marian,Ordinary Time,Easter,Easter,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary TimePrayers of the Faithful
Chorus

Niko katikati ya mbingu na ardhi,

Ninaning'inia sina pa kushika

Duniani sipo na mbinguni sipo

Ninawayawaya Bwana niokoe

Chorus

n/s/ Nikienda huku mambo moto moto

Nikienda kule ni baridi tupu

Mbele yangu giza, nyumba yangu giza

Mahubiri mengi yananiyumbisha imani

Chorus

n/a/ kumtafuta Mwokozi

Ee Mungu wangu uko wapi, ili nije kwako hima,

Mbele yangu kuna giza nene, na nyuma yangunni giza, mahubiri mengi yamezidi

Na mengine yananiyumbisha imani

Chorus

n/t/ Nikienda huku ninabatizwa nannikirudi (kule) ninaitwa mimi kafiri

Giza pande zote mahubiri ni mengi

Na mengine yananiyumbisha imani

Chorus

n/b/ nikienda huku ni moto nikirudi huku baridi

Vuguvugu haitakiwi na imani yangu yayumba

Mungu wangu nisaidie niokoe nisipotee

Mahubiri mengi

Na mengine yananiyumbisha imani

Verse 6

Manabii wengi wananiyumbisha,

Nifuate yupi nimuache yupi

Wapo wa uongo, wapo wa kweli,

Njoo Bwana Yesu Rudi kwetu hima

Ulimwengu huu ulioufia umekuwa Jela la maskini

Verse 7

Roho yangu Bwana inakutamaninwewe peke yako ndiwe tiba yangunneno lako Bwana litaniponya

Kwa sababu wewe Mungu ni mmoja

Twakuomba Baba utuunganishe

Matabaka yote na yatoweke