SectionsThanksgivingIkulu Ya Mbinguni

Ikulu Ya Mbinguni

Ordinary Time,Ordinary Time,Lent,Resurrection,Ordinary TimeThanksgiving
Chorus

{ Ukimcha Bwana Mungu (katika) maisha yako yote

Hakika utakaribishwa (kwenye) ikulu ya Mbinguni } *2

Verse 2

Tazama Mungu ni hodari (sana) wala hamdharau mtu yeyote

Naye ana uwezo (mwingi) katika kufunza ufahamu mwingi

Verse 3

Hufungua masikio (yako) yasikie maonyo yake mwenyezi

Na kukuagiza (urudi) kwake na kuuacha uovu wako wote

Verse 4

Kama wewe ukisikia (wewe) na kumtumikia atapitisha siku zako

Na mafanikio (mengi) na miaka yenu katika furaha

Verse 5

Na ukithamini zaidi (mali) kuliko roho yako utaangamia

Na kufaa pasipo (maarifa) hautauona uso wa Mungu

Verse 6

Basi jitunze isije (hasira) ikakuvuta ama ukafanya mzaha

Wala usikubali (kamwe) ukuu wa ukombozi ukutawale