Chorus
Huruma Bwana, huruma kwa watu wako
Uliowakomboa kwa damu yako takatifu *2
Verse 2
Ee Mungu unirehemu,
Sawa sawa na fadhili zako.
Verse 3
Kiasi cha wingi wa rehema zako,
Uyafute makosa yangu.
Verse 4
Unioshe kabisa na uovu wangu,
Unitakase dhambi zangu.
Verse 5
Ee Mungu uniumbie moyo safi,
Uifanye upya roho uliyotulia ndani yangu.
Verse 6
Usinitenge na uso wako,
Wala Roho wako Mtakatifu usiniondolee.