SectionsBible ProcessionHubirini Viumbe Vyote

Hubirini Viumbe Vyote

Christmas,Christmas,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary TimeBible Procession
Verse 1

Hubirini viumbe vyote muishio duniani

Tangazeni wokovu wake muumba mbingu na nchi

Kwa kuwa Bwana katupenda katuumba

Kwa mfano na sura yake Mungu wetu

Chorus

Hubirini kwa kuimba tena kwa kusali na kucheza

Tangazeni utukufu wake aliye mtawala, Semeninkwa shangwe pia na furaha Bwana ni mtawala

Ametukomboa ametubariki njooni tufurahi naye

Verse 3

Tukuzeni sifa zake enyi viumbe wa duniani

Wahubiriini mataifa habari za utukufu

Kwa kuwa Bwana katupenda katuumba

Kwa mfano na sura yake Mungu wetu

Verse 4

Na nyimbo nzuri na pia shangwe asifiwe Mwokozi

Shamra shamra vigelegele asifiwe Mwokozi

Kwa kuwa Bwana katupenda katuumba

Kwa mfano na sura yake Mungu wetu

Verse 5

Vilema bubu na viziwi wote wapone leo

Matajiri na maskini wote waungane pamoja

Kwa kuwa Bwana katupenda katuumba

Kwa mfano na sura yake Mungu wetu

Verse 6

Watu wote na wasimame washikane mikono

Watoto nao kwa pamoja tuwainue juu

Kwa kuwa Bwana katupenda katuumba

Kwa mfano na sura yake Mungu wetu