Hubirini Kwa Sauti
Christmas,Christmas,Ordinary Time,Ordinary TimeBible Procession
Chorus
Hubirini kwa sauti ya kuimba, tangazeni haya
Hubirini kwa sauti ya kinanda, tangazeni haya
Yatamkeni, tamkeni hadi mwisho wa dunia
Semeni Bwana amelikomboa taifa lake
Verse 2
Mwimbieni Bwana wimbo ule mpya,
Mwimbieni Bwana enyi mataifa
Mwimbieni Bwana kwa sauti ya shangwe,
Mwimbieni Bwana libarikini jina lake
Verse 3
Tangazeni wokovu siku kwa siku,
Hubirini habari za utukufu
Yahubirini mataifa sifa zake,
Na watu wote habari za ukuu wake
Verse 4
Mpeni Bwana utukufu na nguvu,
Mpeni Bwana enyi wana wa Mungu
Pelekeni habari zake pande zote,
Mpeni Bwana utukufu wa jina lake
Verse 5
Mwabuduni Bwana kwa utakatifu,ntetemekeni mbeleze nchi yote
Semeni kwamba Bwana ametamalaki,
Atawahukumu watu wake kwa adili