Hodi Wachunga

ChristmasThanksgiving
Verse 1

Hodi wachunga, msiwe na woga

Amkeni upesi, Bethlehemu mje nasi

Alipozaliwa Mwokozi wenu

Verse 2

Haya twendeni, yumo pangoni

Nyasi alalia alowashukia

Mwenyeji wa mbingu Mwokozi wenu

Verse 3

Pamoja naye mna mamaye

Yeye na Yosefu, mlinziwe mtukufu

Wamtunza kitoto, Mwokozi wenu

Verse 4

Mtukufu Mungu katika mbingu

Na kwenu amani kwa watu amani

Wenye kumwungama Mwokozi wenu

Verse 5

Wakristu nyie twende na siye

Kwenye mwana mchanga kama`o wachunga

Nasi tumwabudu Mwokozi wetu