Chorus
Hodi hodi nyumbani mwako Bwana, ninabisha nifungulie
Nimekuja nyumbani mwako leo, nimekuja kukuabudu,
Kwa unyenyekevu naijongea, meza yako yenye baraka
Nakuja na sala zangu Ee Bwana, nakuomba zisikilize
Ninakutolea sadaka safi, Mungu Baba uipokee.
Verse 2
[ b ] Nyua za Bwana zapendeza, zinapendeza macho kama nini
Natamani kuingia hekaluni, [ w ] nikamwabudu
Verse 3
Nimeingia hekaluni, nimeingia hekaluni mwako
Nimekuja kuabudu kusujudu, nyumbani mwako
Verse 4
Unipokee Mungu wangu unitakase, mimi mwenye dhambi
Nimekuja mbele zako Mungu Baba, unipokee