Hima Hima Najongea

Lent,Ordinary Time,Ordinary Time,Marian,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Lent,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary TimePresentation of Gifts
Chorus

{ Hima hima leo, najongea kwako Bwana,

Ninakuja kwako kwa unyenyekevu wangu,

Nakuletea matunda ya jasho langu,

Pokea Baba nami unipe Baraka } *2

Verse 2

[ t ] Kwa ukarimu nimejitolea mimi mwenyewe,

Polepole nasonga mbele nifike kwako,n[ w ] Nikukabidhi nilicho nacho, hiki kidogo Baba pokea.

Verse 3

Mapato yangu ni duni sana, we wanijua,

Sina kitu kizuri cha kukuletea wewe,

Nakukabidhi maisha yangu, uzima wangu Baba pokea.

Verse 4

Mungu wangu ninakuja kwako nikushukuru,

Umenilinda siku zote asante sana,

Mavuno yangu nakupa wewe, na fedha zangu Baba pokea.

Verse 5

Wiki nzima umenijalia uhai bure,

Umenikinga na matatizo unanipenda,

Mkate huu nakutolea, divai hii Baba pokea.

Verse 6

Baraka zako ninazipokea siku kwa siku

Mungu Baba nionyeshe Mbingu nifanye kazi,

Mifugo yangu nakuletea, furaha yangu Baba pokea.