SectionsExitHiki Kiza

Hiki Kiza

Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Lent,Lent,Ordinary TimeExit
Verse 1

Hiki kiza ni kiza kinene kimetanda ulimwenguni

Kimeyatikisa mataifa makabila mbalimbali

Familia hata majirani makabila hawaelewani

Ofisini hata makazini amani hakuna tena

Chorus

Twalia twaomba amani (amani amani)

Twaomba amani twaomba amani, amani, amani

Watu wengi sasa wameangamia

Wazee watoto nao wateseka

Amani haipo tena duniani Bwana twaomba amani

Verse 3

Pande nyingi watu wamekufa sababu yake ni mizozano

Majirani hawaelewani sababu ya ukabila

Imekuwa sasa kawaida watoto kuwadharau wazazi

Kusema eti wazazi wao wamepitwa na wakati

Verse 4

Migogoro watu mbali mbali taifa na taifa lingine

Wanadamu sasa ni wakali hata kuliko wanyama

Msamaha tumeusahau amri za Mungu tumeziacha

Kila mtu ajiona yeye sasa tutakwenda wapi

Verse 5

Sikieni taifa la Mungu ujumbe huu twawapatia

Mambo haya tunayoyafanya siku moja tutalipa

Mwisho wetu utakapofika utajibu nini kwa Mungu

Atakapotuhukumu sisi kila mtu kadiri yake