SectionsEntranceHii Ndiyo Siku

Hii Ndiyo Siku

Lent,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Marian,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary TimeEntrance
Chorus

Hii ndiyo siku, aloifanya Bwana *2

Tuishangilie, na kuifurahiya *2n{Tupige makofi na vigelegele

Sote turuke juu tumshukuru Mungu } *2

Verse 2

Ndiwe Mungu wangu nami nitakushukuru

Ndiwe Mungu wangu nami nitakutukuza

Nitakushukuru kwa moyo wangu wote

Kwa mema yote Bwana uliyonijalia

Verse 3

Nifungulieni malango ya haki,

Nitaingia mimi na kumshukuru Mungu

Nitakushukuru kwa moyo wangu wote

Kwa mema yote Bwana uliyonijalia

Verse 4

Mkono wa kuume wa Bwana umetukuzwa

Mkono wa Bwana hutenda makuu

Nitakushukuru kwa moyo wangu wote

Kwa mema yote Bwana uliyonijalia

Verse 5

Mshukuruni Bwana kwa kuwa yeye ni mwema

Kwa maana fadhili zake ni za milele

Nitakushukuru kwa moyo wangu wote

Kwa mema yote Bwana uliyonijalia