Chorus
{ Amkeni wote tupeleke vipaji vyetu, (twende)
Tusizifukie talanta tulizopewa } *2
Verse 2
Hesabuni hatua zenu moja mbili tatu,
Tembeeni tukamtolee Mwenyezi vipaji vyetu
Verse 3
Simameni wote onyesheni upendo wenu (kweli)
Na uaminifu katika mioyo yenu
Verse 4
Mwambieni Mungu twakushukuru kwa mema yako (yote)
Ulotujalia katika maisha yetu
Verse 5
Ewe mwanadamu ukumbuke kumshukuru (Mungu)
Umshukuru Mungu wako kwa kila jambo