SectionsExitHazina Ya Mvivu

Hazina Ya Mvivu

Ordinary Time,Ordinary Time,MarianExit
Chorus

Hazina ya Mvivu ni maneno ya uongo (na tena)

Furaha ya mvivu ni kugombanisha watu

Verse 2

Hawezi kulala kapata usingizi usiku

Usiku mzima hukodoa macho akiwaza

Kukipambazuka aende kwa nani kupiga umbeya

Verse 3

Asubuhi mapema huamka na kuvaa nguo

Hajafagia nyumba huyo huyo kwa jirani kaenda

Hodi jirani jirani naye karibu tupo unasemaje

Atapiga umbea hapo hadi chakula cha mchana ale

Verse 4

Akipitapita mitaani huwa amependeza

Salamu kwa watu utasema huyu ni mtu mwema

Kumbe ni muovu asiye kuwa na aibu kwa watu

Verse 5

Wenzake wanaamka mapema na kwenda kazini

Yeye akiamka huyo huyo safari kwenye pombe

Akishafika huko tazama anavyolewa wala hawazi

Familia yake itakula nini mchana na usiku