SectionsExitHawa Ndiyo Wanaotapatapa

Hawa Ndiyo Wanaotapatapa

Christmas,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Marian,Ordinary Time,Easter,Ordinary Time,Ordinary Time,Marian,Ordinary Time,Wedding,Wedding,Wedding,Wedding,Ordinary Time,Wedding,Wedding,Ordinary Time,Ordinary Time,Marian,Ordinary Time,MarianExit
Verse 1

Hawa ndio wale wasiomkumbuka Mungu

Ndio wale wasiomtumaini Mungu

Wanataka maisha ya mkato pasipo kutoka jasho

Hutamani visivyo vyao viwe vyao

Tegemeo lao ni kwa waganga ambapo hupewa dumba

Ili wapate kudhulumu vya wenzao

Verse 2

Hawa ndio wale wanaotapatapa ovyo

Ndio wale wasiomtumaini Mungu

Kila siku ni kiguu na njia eti wasaka pesa

Hata kukumbuka kusali hawataki

Wamesahau ya kwamba Mwenyezi ndiye mgawa vyote

Na ndiye mpaji wa vyote kwa wanawe

Verse 3

Hawa ndio wale wanaomkufuru Mungu

Ndio wanaochezea Jina lake Mungu

Wanaishi maisha ya uzinzi pasipo kufunga ndoa

Na maisha yao hujaa machungu mengi

Wengine wanaharibu miili eti wawe warembo

Kana kwamba Mungu hakuwaumba vizuri

Verse 4

Hawa ndio wale wanaomdhihaki Mungu

Ndio wale wasioheshimu uhai wao

Wanatumia vibaya miili yao kwa ukahaba

Eti ili wajipatie kitu kidogo

Wengine wanavyolegeza ndoa sababu ya nyumba ndogo

Na kuziacha familia zikiteseka

Verse 5

Hawa ndio wale wanaompendeza Mungu

Ndio wale wanaoshika njia zake Mungu

Wale walioyatoa maisha yao kuwa sadaka

Kwa kumtumikia Mungu kwa undani

Wanaouthamini uhai wao pia na majirani zao

Wakisaidiana vyema na kupendana