Chorus
Hakuna aliye sawa naye Mungu
Aketiye mahali patakatifu pake
Anayetutendea mengi makuu ya ajabu
Basi yatupasa sote tumshukuru *2
Verse 2
Ardhi yarutubishwa na mvua zinyeshazo-
Kazi hiyo ni ya nani?
Angalieni mazao yastawi mashambani-
Kazi hiyo ni ya nani?
Verse 3
Watoto wanazaliwa na kukua nazo afya-
Kazi hiyo ni ya nani
Wazazi wapata riziki kuwahudumia-
Kazi hiyo ni ya nani
Verse 4
Safari zawa salama bila misukasuko-
Kazi hiyo ni ya nani
Tumshukuru kwa kuwa yeye ndiye mwenye haki-
Mapenzi yake yatimizwe