Chorus
Ewe Mama wa Mwokozi, tusikie wanao
Tunaotoa machozi, kuomba hurumayo
Tuwe wetu muombezi, kwa Yesu mwanao
Maria Mwema tusaidie
Tuwe wetu muombezi, kwa Yesu mwanao
Maria Mwema tusaidie
Verse 2
Utuombee Maria, sisi wana wa dunia
Tunaosongwa sana na maovu
Verse 3
Kwa kuwa wewe ni Mama, Yesu akupenda sana
Atalisikiliza ombi lako
Verse 4
Utuombee kwa Yesu, asafishe dhambi zetu
Ili tupate heri ya milele