Chorus
{ Enyi wakristu wapenzi njooni
Bwana anatualika kwenye karamu } *2
Kwanza ndugu tazama meza yake inavyopendeza
Yeye Bwana na wateule wameizunguka meza yake
Haya ndugu simama nawe ushiriki *2
Verse 2
Njoni Bwana atuita meza yake sasa itayari
Haya simama nenda nawe ushiriki
Verse 3
Kama wewe wastahili fanya hima ukampokee
Ndicho chakula chenye uzima milele
Verse 4
Yeye anilaye mimi atakuwa na uzima mpya
Siku ya mwisho mimi nitamfufua
Verse 5
Yeye katuandalia masikini pia matajiri
Ukarimu gani Bwana Yesu alionao