Endeni Msiogope
Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Marian,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Marian,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Marian,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Marian,Lent,Ordinary Time,Ordinary Time,Easter,Ordinary Time,Marian,Ordinary Time,Ordinary Time,Marian,Ordinary Time,Ordinary Time,Marian,Ordinary Time,Lent,Ordinary TimeBible Procession
Chorus
{ Enendeni, nendeni msiogope
Lihubiri neno duniani pote, nendeni }*2
Verse 2
Enyi wanafunzi wangu mimi nawatuma
Mataifa yote nendeni mkahubiri
Nendeni kwa moyo wote wala msiogope
Shikeni vyema shauri ninalowapa ee!
Verse 3
Enjili hii viumbe vyote visikie
Ili mapenzi ya Baba yatimilike
Nyumba, anasa na mali havina nafasi
Ondokaneni na hivyo nimewatuma ee!
Verse 4
Dhiki hatari na shida havitawaweza
Giza na hila za mwovu vitayeyuka
Elewa kwamba mimi nipo nanyi daima
Ondoeni shaka kwani sitawaacha ee!
Verse 5
Nanyi mkishatimiza niliyowamuru
Posho kupata na taji mtavalishwa
Itakuwa heri gani Mbinguni kufika
Enzi nitakayopewa kuwarithisha ee!