SectionsEucharistEe Yesu Unihurumie

Ee Yesu Unihurumie

Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Marian,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Marian,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Marian,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Marian,LentEucharist
Verse 1

Ninakuungamia Mungu wangu mpendwa wangu,

Tazama najilaza miguuni kwa majuto

Ee Bwana ninakuomba unitazame kwa huruma

Nalia nahuzunika kwa kuwa mimi nimwenye dhambi

Ni mambo ya ovyo ovyo na upuuzi zinaniponza

Kupenda mambo ya giza, hasira wivu, kiburi choyo

Verse 2

Ee Bwana ninakiri udhaifu wangu wo-te,

Unaujua wazi sidiriki kudanga-nya,

Na sasa naona haya kwa dhambi nyingi nilizo nazo,nnachoka kuishi ji-nsi nilivyo ninaona uchungu.

Unihurumie, unisamehe Bwana ninaumia,nninasikitika ho-fu ni kubwa mwili hauna nguvu.

Verse 3

Popote nipitapo watu hunisema sa-na,

Ni wengi hunifyonya hutikisa vichwa vya-o,

Ni maisha gani haya tazama Bwana yanavyotisha,nsina mbele wala nyu-ma mi-mi kweli ninashangaza.

Tamaa za mwili ona zinavyoiangamiza roho,nadhabu inayoku-ja hakika ni ngumu kuitaja.

Verse 4

Ee Yesu ulikufa kwa ajili yangu mi-mi,

Lakini ona sasa nilivyochanganyiki-wa,

Si m--tu si mnyama ninasi-kitisha sana,nwanyama ndege sama-ki wadudu nao wanashangaa.

Wanataka kunitenga sijui sasa niende wapi,

Ee Yesu nihurumi-e nisaidie mwokozi wangu.

Verse 5

Ee Yesu ndiwe nguvu kwa wanyonge na dhai-fu,

Naomba unigeuze niwe mtu mnyo-fu,

Niuvue mwili mwovu na kwa hasira utupwe mbali,nni maisha gani ha-ya taabu nyingi huzuni tele.

Niwavute watu wengi wakufuate mwokozi wangu,nna mwisho nifike kwa-ko kwenye furaha uzima tele.