Verse 1
Ee ndugu peleka talanta yako kwa Bwana
Kwani Mungu alikupatia kwa kiasi chako
Nawe mrudishie Bwana kama wale watumishi
Kama wale waliopewa talanta mbili na tano
Verse 2
Kumbuka waliopewa talanta mbili na tano
Walileta mbili na tano faida
Bwana wao akawasifu kwa uaminifu wao
Akawapokelea nao akawakweza
Verse 3
Kumbuka aliwapatia tunzo la ufalme
Kwa hao waaminifu kwa hayo machache
Nao wakapewa yaliyo makubwa kwa bwana wao
Na sisi tupeleke talanta zetu kwa Bwana
Verse 4
Kumbuka Mungu alivyokupatia kwa wiki nzima
Atataka kufanya hesabu nawe
Ukumbuke kutoa hesabu kama wale wawili
Naye Bwana Mungu wako atakupokelea