Chorus
Ee Mungu wangu mfalme nitakutukuza
Nitalihimidi jina lako milele na milele
Verse 2
Bwana ana fadhili ni mwingi wa huruma
Si mwepesi wa hasira ni mwingi wa rehema
Bwana ni mwema kwa watu wote
Na rehema zake zi juu ya kazi zake zote
Verse 3
Bwana kazi zako zote zitakushukuru
Na wacha Mungu wako watakuhimidi
Wataunena utukufu wa ufalme wako
Na kuuhadithia uweza wako
Verse 4
Ili kuwajulisha watu matendo yake makuu
Na utukufu wa fahari ya ufalme wake
Ufalme wako ni ufalme wa zamani zote
Na mamlaka yako ni ya vizazi vyote