SectionsExitEe Mungu Jina Lako

Ee Mungu Jina Lako

Ordinary TimeExit
Chorus

Ee Bwana Mungu jina lako ni tukufu sana

Duniani na mbinguni wewe watawala! (pia*2)

Nikiziangalia mbingu kazi ya vidole vyako

Mwezi pia na nyota Bwana umeratibisha wewe

Wanyama wa porini, ndege, samaki warukaruka!n(Njooni) njooni tumwimbie Bwana

Njooni tumwimbie Bwana, yeye ameumba vyote

Njooni tumwimbie *2 njooni tuimbe na ngoma

Piga na zeze vinanda ametuumba njooni tumwimbie}

Verse 2

Kaumba nchi (kaumba wanyama)

Samaki wa baharini(-rini na ndege)

Vyote hivyo vyapendeza (-ndeza kama nini)

Njooni imbeni (njooni tumwimbie)

Verse 3

Mimea yote (ameumba yeye)

Nchi yote ikajaa misitu

Chakula chao wanyama (ni matunda yake)

Nyama na ndege wanaruka (-ruka angani

Verse 4

Tazama mtu (ndiye kitu gani)

Hata wewe umkumbuke (-mbuke ee Bwana)

Na binadamu ni nani (nani ee Bwana)

Umwangazie (kwa wema)