Ee Mariamu Wafahamu
Marian,Ordinary TimeThanksgiving
Verse 1
Ee Mariamu wafahamu, wanao wa ugenini
Tupe, Mama, usalama,
Utulinde hapa chini, utulinde hapa chini
Verse 2
Nyota nzuri ya bahari, tuliza dhoruba mbaya,
Na za mwovu, vunja nguvu,
Simwache kutuogofya, simwache kutuogofya
Verse 3
Na memayo jaza nyoyo, za mayatima waombi
Utukaze tuongoze,
Tusichafuke na dhambi, tusichafuke na dhambi
Verse 4
Tukitishwa tukisongwa, na ya mwisho masumbuko
Uje hima na ujima,
Kuopoa watoto wako, kuopoa watoto wako
Verse 5
Ukaako wana wako, Maria Mama Bikira,
Uwinguni kwa amani,
Waonje furaha bora, waonje furaha bora