SectionsExitEe Malkia Wa Mbingu Ufurahi

Ee Malkia Wa Mbingu Ufurahi

EasterExit
Chorus

Ee malkia wa mbingu Maria ufurahi aleluya

Amefufuka mkombozi amefufuka

Kwani mwanao uliyemchukua ametoka kaburini

Amefufuka mkombozi tufanye shangwe

Verse 2

Mauti ameyashinda Mwokozi amefufuka

Kuzimu ameshatoka Kristu na yuko hai

Shetani ameumbuka na dhambi imefutika

Verse 3

Ni kweli alivyosema ya kwamba angekamatwa

Ateswe mpaka kufa lakini angefufuka

Na sasa amefufuka ushindi tumeupata

Verse 4

Wakristu tuudumishe uhuru tuliopata

Kwa damu aliyomwaga Mwokozi msalabani

Tuache madhambi yetu tudumu katika neema