SectionsThanksgivingEe Bwana Wangu

Ee Bwana Wangu

Ordinary Time,MarianThanksgiving
Chorus

Ee Bwana wangu na muumba wangu,

Wema wako wanitia nguvu kuongea nawe

Ee Mungu wangu u tumaini langu,

Wewe ni mlinzi mwaminifu wa maisha yangu

Ninajua wazi ya kwamba, unanipenda upeo Bwana

Wewe ni mwali mwangavu wa roho yangu

Ndiwe tegemeo pekee, ni kimbilio langu, Bwana,

Chanzo cha uzima wangu, na ngome yangu

Verse 2

Kama sio wewe Bwana kukaa pamoja nami,

Wanadamu waliponishambulia wangenimaliza

Ulikuwa ngao yangu, Mwokozi wa roho yangu

Sina budi kusema asante naomba usiniache

Verse 3

Nilipokuita Bwana uliitika mapema

Katika taabu zangu zote ulituma jeshi lako

Umenifanya imara imani sikuitupa

Na leo tazama niko hapa kutaja uwezo wako

Verse 4

Ni kweli naona wazi huruma uliyo nayo

Umenisamehe dhambi zangu ingawa ni chafu sana

Umenitoa shimoni umenifuta machozi

Naomba unipake mafuta nieneze sifa zako

Verse 5

Nitakupa nini Bwana kama shukrani zako,

Kwa ukarimu uliotenda, katika maisha yangu

Umeniokoa Bwana, minyororo imekatwa

Naomba usinitupe Bwana, shetani ananiwinda