SectionsExitEe Bwana Unikumbuke

Ee Bwana Unikumbuke

LentExit
Chorus

(Ee Mwana wa Mungu unifanye leo nishirikinkwenye karamu yako karamu ya kiroho )* 2n(Sitaifunua siri kwa adui zako

Wala mimi sitakupa busu kama lile la Yuda) * 2

Bali kama yule mwizi

Ninakuomba ee Bwana unikumbuke mimi katika ufalme wako

Verse 2

Ninakuabudu Bwana kifulifuli,

Enzini uliyefichika Mungu uliye hai

Ulipo kweli chini ya maumbo haya,

Ya mkate pia divai ninajinyenyekeza

Karibu kwangu Bwana njoo ukae nami

Verse 3

Huu ni mwili na damu kweli ni hakika

Nikiona nigusa tena nikionja

Ni Yesu mwenyewe mimi pia ninasadiki

Aliyejitoa kwa ajili ya ulimwengu

Fumbo hili ni la kweli imani inaelewa

Verse 4

Kila ninapopokea komunyo takatifu

Ninarudishiwa nguvu mpya bila shaka

Ekaristi huimarisha mapendo moyoni

Yadumisha amani furaha iliyopotea

Hii hakika ni dawa safi ya roho